ULIPAJI WA ADA KWA JUMUIYA ZA KIRAIA ZILIZOSAJILIWA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Ofisi ya Msajili wa Jumuiya Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi inazikumbusha Jumuiya za Kidini
na zisizokuwa za Kidini zilizosajiliwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kulipa
Ada ya Mwaka pamoja na malimbikizo ya ada za miaka ya nyuma kabla ya tarehe
30/6/2023.
Jumuiya za Kidini zinapaswa kulipa Ada ya Shilingi
100,000 na Jumuiya zisizo za Kidini zinapaswa kulipa Ada ya Shilingi 50,000.
Aidha, ulipaji wa ada unapaswa kwenda sambamba na uwasilishaji wa Taarifa za Fedha
zilizokaguliwa na Taarifa za Utendaji za
Jumuiya hizo kwa kipindi cha mwaka 2022/2023.
Viongozi wa Jumuiya zote zilizosajiliwa wanakumbushwa
na kusisitizwa kutumia Mfumo wa Usajili na Usimamizi wa Jumuiya (RSMIS)
unaopatikana kwenye tovuti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambayo ni www.moha.go.tz
kwa ajili ya kulipa Ada za Jumuiya zao au kufika katika Ofisi zetu zilizopo Jengo
la Kambarage Ghorofa ya 11 Jijini Dodoma au Jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi Ghorofa ya Kwanza Jijini Dar es salaam kwa lengo la kupatiwa huduma
stahiki.
Kwa maelekezo zaidi, piga simu namba 0734
712 744 au 0734 712 745.
Imetolewa na:
Emmanuel
R. M. Kihampa
MSAJILI WA JUMUIYA ZA
KIRAIA