ZOEZI LA UHAKIKI NA UHUISHAJI WA VYETI VYA USAJILI WA TAASISI ZOTE ZA DINI
TANGAZO
Ofisi ya Msajili wa Jumuiya, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, itaendesha Zoezi la Uhakiki na Uhuishaji wa Vyeti vya Usajili wa Taasisi zote za Dini zilizosajiliwa na Wizara hii.
Zoezi limeanza tarehe 21 Novemba 2022 hadi tarehe 3 Desemba 2022 katika Kanda ya Mashariki inayohusisha Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro. Tarehe za Mikoa mingine zitatangazwa baadae.
Zoezi litafanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar es Salaam kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni.
Viongozi wa taasisi za kidini wanasisitizwa kufika kwenye Kituo cha Kuhakiki na Kuhuisha Vyeti vya Usajili, wakiwa na
· Cheti cha Usajili pamoja na Nakala ya Cheti hicho,
· Katiba na Kanuni zinazotumiwa na Taasisi za Dini kwa sasa
· Taarifa za Mapato na Matumizi na Utendaji kwa kipindi cha Miaka mitano iliyopita,
· Uthibitisho wa Malipo ya Ada kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, na
· Ada ya shilingi 100,000/= kwa ajili ya kupatiwa Cheti kipya.
Taasisi za Kidini zitakazoshindwa kushiriki zitahesabika hazipo hai hivyo kujiondoa zenyewe kwenye Kazindata ya Jumuiya zilizosajiliwa.
Huduma za Ulipaji wa Ada ya Mwaka, Uwasilishaji wa Maombi Mapya ya Usajili zitatolewa katika Vituo vya Uhakiki. Kanda itakayofuata ni Kaskazini na baadae Kanda ya Ziwa hivyo Viongozi wa taasisi za Dini wajiandae.
Kwa maelezo na ufafanuzi zaidi wasiliana na Ofisi ya Msajili wa Jumuiya kupitia namba ya simu +255734712744, +255734712745 au barua pepe rs@moha.go.tz.
Imetolewa na:
MSAJILI WA JUMUIYA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI