Ofisi ya Msajili wa Jumuiya imeanzishwa mwaka 1955 chini ya Sheria ya Jumuiya Sura ya 337, Ofisi hii ipo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Ofisi ya Msajili wa Jumuiya ina wajibu wa kusajili na kusimamia Jumuiya zote za Kidini na zisizokuwa za Kidini Tanzania Bara.
Aina ya Jumuiya zinazosajiliwa katika Ofisi hii zimegawanyika katika Nyanja kuu tano ambazo ni Jumuiya za kidini, kitaaluma, Kijamii, kiuchumi na kiutamadani.