RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan, amevifungua Vituo Vikuu vya Polisi vya Wilaya ya Ikungi na Mkalama Mkoani Singida, leo Oktoba 15, 2023. Baada ya ufunguzi huo, Rais Samia amempongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi kwa kusimamia vema ujenzi wa vituo hivyo vya Polisi Mkoani humo.