Tanzania logo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

ZOEZI LA USAJILI WA JUMUIYA KATIKA MKOA WA MBEYA KUANZIA TAREHE 01 MPAKA 05 JULAI, 2024

TAARIFA KWA UMMA

 

ZOEZI LA USAJILI WA JUMUIYA KATIKA MKOA WA MBEYA KUANZIA TAREHE 01 MPAKA 05 JULAI, 2024

 

 

Ofisi ya Msajili wa Jumuiya, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi itaendesha Zoezi la Usajili wa Jumuiya ikiwemo vyama na vikundi vya Kiuchumi, Kitamaduni, Kitaaluma na Kijamii vilivyopo katika jiji la Mbeya. Zoezi hilo linatarajiwa kuanza tarehe 01 hadi 05 Julai, 2024 jijini Mbeya.

 

2.              Kituo cha usajili kitakuwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya. Aidha, vyama na vikundi vinavyoomba usajili vitapaswa kufika katika kituo cha usajili vikiwa na nyaraka zifuatazo:

         i.         Barua ya utambulisho kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya;

        ii.         Orodha ya majina ya Wanachama Waanzilishi ikiwa na saini zao;

      iii.         Wasifu (CV) wa viongozi Wakuu wa Jumuiya husika  ukiwa umebandikwa picha moja  (passport size);

      iv.         Katiba na Kanuni za Jumuiya (kama zipo) na muhtasari wa kikao kilichopitisha katiba na kanuni ukiwa na majina na saini za wajumbe waliohudhuria kikao hicho;

       v.         Ada ya maombi ya usajili Shilingi 50,000/=, Malipo ya cheti cha usajili Shilingi 100,000/= na Ada ya mwaka Shilingi 50,000/= . Jumla ya gharama za usajili ni shilingi 200,000/=.

3.              Vikundi vya kijamii vilivyopo katika Mikoa ya karibu kama vile Iringa, Njombe Songwe na Rukwa wanaalikwa kutumia fursa hiyo kwa ajili ya kusajili vikundi vilivyopo katika maeneo yao.

4.              Kwa msaada na huduma zaidi Kwa maelezo na ufafanuzi zaidi tafadhali piga namba za simu 0734712744, 0734712745 au tuma barua pepe kwenda anuani rs@moha.go.tz.

 

Imetolewa na:-

 

MSAJILIWA JUMUIYA ZA KIRAIA