Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
Mkimbizi ni mtu yeyote ambaye kutokana na hofu ya msingi ya
kuteswa kwa sababu za rangi, dini, kabila, uanachama wa kundi la kijamii au
maoni ya kisiasa, yuko nje ya nchi yake au nchi ya maskani yake ya kudumu na
kwamba hawezi au hayuko tayari kuwa chini ya himaya ya serikali hiyo ambayo
ameikimbia.
A refugee is any person whom owing to well-founded fear
from persecution for reasons of race, religion,
ethnicity, nationality, membership a of particular social group or political
opinion is outside his country of nationality or habitual residence and is unable
or unwilling to avail himself to the protection of the government which he has
previously fled.
Mhamiaji haramu ni raia
wa kigeni aliye ndani ya Tanzania na asiye
na kibali halali cha kuingia au kuishi Tanzania wakati mkimbizi ni raia wa nchi
ya kigeni aliyeomba na kupewa hifadhi kutokana na kuikimbia nchi yake kwa
sababu za usalama wake
Illegal immigrant is person who is in Tanzania without the
legal right to live or to be in the country while a refugee is a person who has
fled from his country for the fear of persecution and has asked asylum and
registered in Tanzania.
Waomba hifadhi wote wanapowasili nchini wanatakiwa kuripoti katika
Ofisi zozote za Serikali ambako wataelekezwa kufika Idara ya Wakimbizi au
kuonana na “Ofisa aliyeidhinishwa” ambaye
atawapa utaratibu wa kufuata kufika Ofisi za Idara ambako watahojiwa na kusajiliwa.
All asylum seekers must report to government
offices upon their arrival in the country. They will be directed to the Refugee
Department or meet with an “authorized officer” who will provide instructions
on how to proceed to the department's offices for their interview and
registration.
Ifahamike kwamba maeneo wanayoishi wakimbizi ni maeneo tengefu, hivyo
wageni wote wanaotaka kuingia katika maeneo haya kwa ajili ya kutoa huduma au
sababu zozote zile; watapaswa kuandika barua ya kuomba kibali kwa Mkurugenzi wa
Idara ya Huduma kwa Wakimbizi. Hairuhusiwi kuingia maeneo tengefu bila kibali.
It should be noted that refugees live
in designated areas, therefore, Visitors who wish
to enter the refugee camps whether to provide services or for any other
purpose, must submit a letter to the Director of the Refugee Services
Department to request for a camp entry permit. It is strictly
prohibited to enter these designated areas without a permit.
Usafirishaji haramu wa binadamu unahusisha kitendo cha
kuajiri, kusafirisha, kuficha au kupokea mtu kwa njia ya vitisho, nguvu,
udanganyifu au matumizi mabaya ya madaraka kwa lengo la unyonyaji. Unyonyaji
unaweza kuwa wa kazi za kulazimishwa, ukahaba, kufanya kazi za ndani, kulazimishwa
kuomba mtaani au kushirikishwa katika vitendo vya uhalifu.
Trafficking in persons involves recruitment, transportation,
harboring, or receiving of a person by any means including threats, force,
deception, or abuse of power for the purpose of exploitation. Exploitation may
include forced labor, sexual exploitation, domestic servitude, forced begging,
or involvement in criminal activities.
Viini vinavyounda kosa la usafirishaji haramu wa binadamu
ni;
· Tendo
Lenyewe: Kusajiri, Kusafirisha, kuhamisha, kuhifadhi, kutoa au
kupokea mtu kwa ajili ya kumtumikisha
· Mbinu:
kudanganya, kutisha au kutumia nguvu, kuteka na kutumia mikataba ya uongo
· Nia/Kusudio:
kutumikisha kingono, kufanyisha kazi ngumu, kulazimisha kuomba mitaani, kutoa
viungo vya mwili na kufanyisha kazi za ndani
Elements that constitute trafficking in persons offence
includes;
- The
act: Recruiting, transporting, transferring,
harboring, giving or receiving a person for purpose of
exploitation.
- The
means: Use of threats, force, fraud, deception,
abuse of power, exploitation of vulnerability, or offering/receiving
payments to gain control over a person.
- The
purpose: Exploitation, such as forced labor, sexual
exploitation, slavery, organ removal, or other forms of abuse.
Ndiyo. Usafirishaji haramu wa binadamu ni kosa la jinai
chini ya Sheria ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu, Sura ya 432.
Wahalifu hukabiliwa na adhabu kali ikiwemo kifungo cha maisha gerezani.
Yes, trafficking in persons is a criminal offense under the
Anti-Trafficking in Persons Act, Cap. 432. Offenders face heavy penalties
including life imprisonment.
Dalili ni pamoja na: haruhusiwi kuondoka sehemu ya kazi,
kunyanganywa nyaraka binafsi, kufanya kazi kwa muda mrefu bila malipo au kwa
malipo kidogo, anakula mabaki ya chakula kilichoachwa na mwajiri wake, ana
makovu au vidonda ambavyo havijatibiwa kutokana na kuteswa, kuonyesha hofu au
wasiwasi uliopitiliza, na kutumikishwa kwenye ukahaba au kazi za kinyonyaji.
Restricted movement, lack of access personal documents,
working long hours with little or no pay, eat leftovers, has scars or un
attended wounds, showing fear or anxiety, being forced into sexual or
exploitative work.
Mtu yeyote anaweza kusafirishwa kiharamu, lakini makundi
yaliyo hatarini zaidi ni wanawake, watoto, watu wenye ulemavu, maskini na
wahamiaji wanaotafuta fursa.
Anyone can be trafficked, but vulnerable groups include women, children, people with disabilities, the poor, and migrants seeking opportunities.
Vichocheo ni pamoja na umaskini, ukosefu wa ajira, mahitaji
ya nguvu kazi ya bei nafuu, ukahaba, migogoro ya kifamilia, ukosefu wa elimu, utandawazi,
tamaa ya maisha mazuri na faida kubwa wanayoipata wahalifu wanaojihusisha na
biashara hii.
Poverty, unemployment, demand for cheap labor, sexual
exploitation, family conflicts, lack of education, globalization, dreams of a
better life and the profitability of trafficking networks.
Magendo kwa wahamaji yanahusisha kuvuka mipaka kinyume cha
sheria kwa ridhaa ya mhusika, na mara nyingi huishia baada ya kuwasili eneo
analokwenda. Usafirishaji haramu wa binadamu unahusisha unyonyaji, mara nyingi
bila ridhaa, na huendelea hata baada ya kufika mwisho wa safari.
Smuggling is illegal border crossing with consent, usually
ending after arrival to the destination. Trafficking involves exploitation,
often without consent, and continues even after transportation.
Kwa Waathirika: mateso, msongo wa mawazo, unyanyapaa,
magonjwa, kupoteza uhuru na kifo. Kwa Familia: utengano, mzigo wa kifedha. Kwa
Taifa: hasara ya kiuchumi, machafuko ya kijamii na kudhalilika kimataifa.
On Victims: abuse, trauma, stigma, diseases, loss of
freedom and death. On Families: separation, financial strain. On the Nation:
economic loss, social instability, and reputational damage.
Kupitia Sheria ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu
(Sura 432), kupitia Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Usafirshaji Haramu
wa Binadamu, kampeni za uelimishaji, mafunzo na ushirikiano na taasisi mbalimbali
zikiwemo za kimataifa.
Through the Anti-Trafficking in Persons Act Cap 432, through
Anti-trafficking in Persons Secretariat, awareness campaigns, training, and
partnerships with national and international stakeholders.
Ripoti mara moja katika kituo cha polisi, piga simu kwenye
namba ya dharura 195 ya Sekretarieti ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu,
au toa taarifa kwa viongozi wa eneo husika.
Report immediately to the police, call the Anti-Trafficking
Secretariat hotline 195, or inform local authorities.
Waathirika hupata msaada wa uokoaji, makazi salama ya muda,
huduma za afya, ushauri, msaada wa kisheria, utafutaji wa familia, msaada wa
kurejeshwa kwenye jamii, na ulinzi wa haki na utambulisho wao.
Victims receive rescue, shelter, healthcare, counseling,
legal aid, family tracing, reintegration support, and protection of identity
and rights.
Kujielimisha, kuripoti matukio yanayotiliwa shaka, kusaidia
familia zilizo hatarini, na kuelimisha jamii kupitia shule, makanisa, misikiti
na mikutano ya kijamii.
Stay informed, report suspicious activities, support vulnerable families, and raise awareness in schools, churches, mosques, and communities.
Tembelea ofisi ya Sekretarieti au tovuti ya Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, fuatilia kampeni za uelimishaji, au piga simu kwa namba ya
dharura 195.
Visit the Anti-trafficking in Persons Secretariat office or
Ministry of Home Affairs’ website, follow awareness campaigns, or call the
national hotline 195.
