Tanzania logo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

NAFASI ZA KUHAMIA KATIKA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

TANGAZO

 

NAFASI ZA KUHAMIA KATIKA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imepewa kibali na mwenye Mamlaka Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora cha kujaza nafasi 26 zilizo wazi kwa utaratibu wa kuhamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 

Kwa kibali hicho Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi anawatangazia watumishi wote wa Umma Tanzania, wenye nia na wanaokidhi vigezo vya Kimuundo kuwasilisha maombi kwa ajili ya nafasi za zifuatazo hapo chini:-

 

1.Msaidizi wa Kumbukumbu Mkuu Daraja II - Nafasi 1,


2.Msaidizi wa Kumbukumbu Mwandamizi - Nafasi 2,


3.Afisa Ugavi Mkuu Daraja la II - Nafasi 1,


4.Afisa Ugavi Mwandamizi - Nafasi 1,


5.Afisa Ugavi Daraja la II - Nafasi  2,


6.Mchumi Daraja la I - Nafasi 1,


7.Mchumi Mwandamizi - Nafasi  2,


8.Mchumi Mkuu Daraja la II - Nafasi 1,


9.Mtakwimu Mkuu Daraja la II - Nafasi 1,


10.Mtakwimu Daraja la I - Nafasi 1,


11.Afisa Ustawi wa Jamii Daraja la II - Nafasi 5,


12.Afisa Hesabu Mwandamizi - Nafasi 1,


13.Afisa Sheria Mkuu Daraja la II - Nafasi 3,


14.Afisa Sheria Mwandamizi - Nafasi 2,


15.Mkaguzi wa Ndani Mwandamizi - Nafasi 1,


16.Mkaguzi wa Ndani Daraja la I - Nafasi 1,           

 

 

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI:

i.Waombaji wote wapitishe barua za maombi kwa Waajiri wao


ii.Maombi hayo yaambatane na uthibitisho wa Mwajiri kuhusu uhakiki wa vyeti vya kidato cha nne kutoka NECTA


iii.Waambatishe maelezo binafsi (CV) yenye anuani zao, namba za simu pamoja na majina ya wadhamini watatu wa kuaminika


iv.Maombi yaambatane na vyeti vya elimu na taaluma


v.Mwombaji asiwe na shauri la kinidhamu


vi.Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 30 Juni, 2024

vii.Mwombaji atajigharamia gharama za uhamisho


viii.Maombi yawasilishwe kupitia Mfumo wa kielektroniki wa Uhamisho e-transfer kwa anuani ya:-

 

Katibu Mkuu,

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,

S. L. P 2916,

40483 DODOMA

 

Imetolewa na: Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi