TANGAZO LA MNADA
TANGAZO LA MNADA
Wananchi wote mnatangaziwa kwamba, Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi itauza kwa njia ya Mnada wa Hadhara Samani, Gari, Mitambo na vifaa
mbalimbali chakavu katika Ofisi zake za Dodoma, Dar es salaam, Tabora na Katavi
kwa tarehe kama ilivyooneshwa hapa chini.
13/Agosti/ 2024 |
Ofisi za Wizara Mtumba - Dodoma |
Meza, Viti, Kabati, Printer, Scanner, UPS, Monitor, CPU |
6/Agosti/2024 |
Ofisi za Wizara - Dar es salaam |
Meza, Viti, Kabati, Printer, Scanner, UPS, Monitor |
16/Julai/2024 |
Makazi ya Wakimbizi Ulyankulu Tabora |
Meza,
Viti, Taa, Jenereta, Printer, Scanner, UPS, Gari aina ya LandRover na Jeep |
19/Julai/2024 Ofisi ya ya Wakimbizi Mkoa wa
Katavi Meza, Viti, Jenereta, Printer, Scanner, UPS, Monitor
MASHARTI YA MNADA
1. Mali
itauzwa kama ilivyo mahali ilipo;
2.
Mnunuzia atalazimika kulipa papohapo (100%)
thamani ya samani/Kifaa alichonunua kama ilivyofikiwa katika mnada. Aidha, kwa
vyombo vya moto Mnunuzi atatakiwa kulipa papohapo amana (deposit) isiyopungua
asilimia ishirini na tano (25%) ya thamani ya Chombo alichonunua, na
kukamilisha malipo yote katika muda wa siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe ya
mnada. Mnunuzi akishindwa kutimiza sharti hili atakosa haki zote za ununuzi wa
Chombo husika na amana iliyolipwa haitarudishwa,
3. Mnunuzi
atatakiwa kuondoa/kuchukua mali aliyonunua mara baada ya kukamilisha malipo;
4. Ruhusa
ya kuangalia mali itatolewa siku moja (1) kabla ya tarehe ya mnada husika;
6. Mnada utaanza saa Nne (04:00) asubuhi katika kila kituo.
Ole-Mbille
Kissioki
KAIMU
KATIBU MKUU