Tanzania logo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

WAZAZI MUWE MAKINI NA WATOTO



Naibu Waziri Wa Mambo Ya Ndani Ya Nchi Mhe.Jumanne Sagini, Amewataka wazazi na walezi Wote Kuhakikisha wanakuwa Makini na Watoto wao Katika Kipindi Hiki Cha Sikukuu Ya Eid El Fitr Ili kuepukana na Majanga Mbalimbali Ikiwemo Kupotea au Kufa Maji.
.
Ameyasema hayo Leo April 22,2023 Alipokuwa amehudhuria katika ibada Ya Eid El Fitri Kwenye Msikiti wa Kichangani -Magomeni Jijini Dar es Salaam.
.
Sagini Amesema Kumekuwa na Matukio Kipindi Cha Nyuma Watu wanapofurahi wanajiingiza Kwenye Maeneo Ambayo hawachukui Tahadhari na Baadae hupelekea Matatizo Makubwa Hasa Kwa Watoto.
.
"Kuna Matukio Yamekuwa Yakitokea Katika Kipindi Cha Nyuma, Watu wanapofurahi wanajiingiza Kwenye Maeneo Ambayo hawachukui Tahadhari yoyote na Madhara huwafika Hasa Watoto wadogo.
.
"Wanapelekwa kwenye Kumbi zisizokuwa na Hewa ya Kutosha, Beach Zisizo na Uangalizi Wa Kutosha na kupelekea Watoto wengine Kufa Maji Au Kupotea" Amesema Sagini.
.
Naibu Waziri Huyo Amewahimiza Wananchi Wote Kusherehekea Sikukuu Ya Eid El Fitr Kwa Hali Ya Usalama, Na Kwa Mtu Yeyote atakayefanya Kitu Kinyume na Maadili Ya Nchi Yetu atachukuliwa Hatua Kali za Kisheria.
.
"Tusingependa Kuchukua Hatua Kali  Kwa Watu, Leo Tulikuwepo Kwenye Ibada Lakini Wakilazimika Kufanya Mabaya Sheria itachukua Mkondo Wake. 
Lakini Leo Siku Ya Furaha, Naimani Kila Mtu Atakwenda Kufurahia". Amesema Sagini.
.
Aidha, Sagini Amewahimiza Waislamu Wote Kuendelea kutenda Mema yampasayo Mwenyezi Mungu hata Kama Mwezi Mtukutu Wa Ramadhan umeisha Bali Waendelee Kuwa Watu wema na Kutenda Mema Kwa Mola Wao.
.
"Mambo Mema Yasiishe Kwa Sababu Mfungo Wa Ramadhan Umekwisha, Watu waendelee Kutenda Yaliyo Mema Kwa Ajili ya Kesho Yao Na Kwa Ajili Ya Mola" Amesema Sagini