Tanzania logo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI KASPAR MMUYA AMETEMBELEA "TPHS" DAR ES SALAAM"



Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kaspar Mmuya leo tarehe 21.04.2023 ametembelea Makao Makuu ya Shirika lisilo la kiserikali la THPS (Tanzania Health Promotion Support) lililopo Coco Plaza, Jijini Dar es Salaam.

Ziara hiyo imelenga kutambua namna ambayo shirika hilo limekuwa likishirikiana na Jeshi la Polisi na Magereza katika kutoa huduma kwa wagonjwa wa VVU na TB kwa wafungwa, mahabusu, maofisa wa Polisi na magereza na familia zao.

Katibu Mkuu Mmuya amesema, licha ya kuwa na changamoto mbalimbali lakini ipo haja kwa shirika hilo kuweka mifumo na jitihada za kupunguza maambukizi mapya ya maambukizi Virusi Vya Ukimwi na kuwalinda watoto wanao zaliwa wasizaliwe na virusi vya Ukimwi ifikapo 2030.

Aidha amesisitiza kuwa katika kukabiliana na kusambaa kwa magonjwa kama TB na UKIMWI ni vizuri kuwekeza katika elimu ya afya, ambapo Katibu Mkuu Mmuya amesema, "nashauri kuwekeza katika elimu kwa watu ili kuweza kujikinga na magonjwa yanayoambukiza kama inawezeka itakuwa vizuri kama itaingizwa katika mitaala ya elimu ili watu wajifunze kuanzia shuleni"

Katika hatua nyingine amezitaka Tasisi zisizo za kiserikali kutojiingiza katika miradi ambayo hailindi mila na desturi za nchi yetu.

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu Ndugu, Mmuya ameongozana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Mzee Ramadhan Nyamka na maofisa wa waandamizi wa Magereza.

Shirika hilo la TPHS linaongozwa na Mkurugenzi Mkuu Dr. Redempta Mbatia, Shirika hilo  linasaidia huduma kamili za kinga, matunzo na matibabu ya VVU na TB katika vituo 64 vya afya  kwa Polisi na Magereza, Tanzania Bara na Zanzibar, katika kuwahudumia wangonjwa wa VVU na TB walio katika mahabusu za Polisi na Magereza. Pia utoaji endelevu wa huduma za afya kwa watumishi wa Polisi na Magereza, familia zao na jamii zinazowazunguka.