Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Ally Senga Gugu ameliagiza Jeshi la Magereza nchini Kuongeza ufanisi katika shughuli zake za uzalishaji ikiwemo kilimo,ufugaji na uzalishaji wa bidhaa za viwandani huku akilitaka jeshi hilo kuhakikisha linazalisha mazao kwa wingi na kuuza ndani na nje ya mipaka ya Tanzania baada ya kukamilisha jukumu la kulisha askari magereza na wafungwa. Ametoa rai hiyo wakati wa Ziara ya Ukaguzi wa Mazao ya Mahindi yaliyovunwa katika Gereza la Kilimo la Songwe na Gereza la uzalishaji wa sabuni katika Gereza la Ruanda mkoani Mbeya.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ally Gugu amehitimisha mafunzo ya Awali ya Askari wapya wa Uhamiaji zaidi ya 500 Kozi Namba 04/2025 Katika Chuo Cha Uhamiaji Raphael Kubaga kilichopo Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga, Oktoba 3, 2025
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Maduhu kazi leo tarehe 01 Septemba 2025 amefungua, Kikao kazi cha Kamishna Jenerali wa Uhamiaji na Viongozi Waandamizi wa Idara ya Uhamiaji Tanzania.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Ally Gugu Leo tarehe 29 Agosti 2025 amefungua na kuzindua Bodi ya kwanza ya utendaji ya Chuo cha Uhamiaji Cha Kikanda Tanzania (TRITA) Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amevihimiza Vyama vya Siasa pamoja na Wagombea wa Urais, Ubunge na Udiwani kunadi sera zao kwa Wananchi bila kutumia lugha ya matusi au kuanzisha vurugu zinazoweza kuhatarisha amani, pia amewasisitiza Wananchi kushiriki katika shughuli za kisiasa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu na kushiriki kupiga kura Oktoba 29, 2025.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameipa heshima nchi kwa kuhamasisha matumizi ya Nishati safi ya kupikia, ambayo ni kipaumbele cha mataifa mengi duniani.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Innocent Bashungwa amezindua Mikakati 6 ya Mawasiliano ya Wizara na Vyombo vya Usalama, 9.1.2025 Dodoma