KATAMBI, KOMBO WAKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA IOM
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo wamekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), Amy Pope ambae ameongozana Mkurugenzi wa Kikanda wa Pembe ya Afrika na Afrika Kusini, Frantz Celestin na Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) Tawi la Tanzania, Ashraf Hassan na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Shirika la Uhamiaji (IOM), Mohammed Abunajela.
Ujumbe wa Tanzania pia umewakilishwa na Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar,Hassan Ali Hassan, Mwakilishi wa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Kamishna wa Divisheni ya Sheria,Novaita Mrosso.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji(IOM), Amy Pope yuko nchini kwa ziara ya kikazi ambapo amekutana pia na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan, tarehe 17/8/2026, Visiwani Zanzibar.
