Tanzania logo
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

MHE. AYOUB ASHIRIKI HAFLA YA MAKABIDHIANO NA UZINDUZI WA BOTI


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, ameshiriki hafla ya makabidhiano na uzinduzi wa boti mbili za kisasa za doria kwa ajili ya kuimarisha usalama katika bahari na Maziwa Makuu, Julai 31, 2026 katika viwanja vya Bandari ya Dar es Salaam.


Boti hizo mpya, PB Sailfish 02 na PB Sailfish 03, zimekabidhiwa kwa lengo la kuongeza uwezo wa kufanya doria na kuimarisha ulinzi wa mipaka ya maji pamoja na kukabiliana na uhalifu katika maeneo ya bahari na Maziwa Makuu.


Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, ambaye ameongoza zoezi la kukabidhi na kuzindua boti hizo.