Kusimamia masuala ya Zimamoto na Uokoaji

Majukumu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ni kukinga na kupunguza idadi ya vifo, majeraha kwa watu, na uharibifu wa mali kutokana na moto, mafuriko, matetemeko, ajali za barabarani na majanga mengine.
Idara na Vitengo vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ni pamoja na:

  1. Divisheni ya Usalama wa Moto;
  2. Divisheni ya Operesheni;
  3. Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu;
  4. Kitengo cha Sheria;
  5. Ofisi za Zimamoto na Uokoaji Mikoa;
  6. Ofisi za Zimamoto na Uokoaji Wilaya;
  7. Vituo vya Zimamoto na Uokoaji na;
  8. Chuo cha Zimamoto na Uokoaji.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linaongozwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji akisaidiwa na Naibu Kamishna Jenerali, Makamishna na Makamanda wengine. Tembelea Idara ya Zimamoto na Uokoaji. www.frf.go.tz

Back to Top