generica viagra

News

LUGOLA ATANGAZA OPERESHENI KUWAONDOA WAHAMIAJI HARAMU MKOANI KIGOMA

Wednesday, October 3, 2018

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, ameitaka Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kigoma ishirikiane na Jeshi la Polisi kufanya operesheni maalum ya kuwaondoa wahamiaji haramu mkoani humo.
 
Akizungumza na mamia ya wananchi katika uwanja wa Mnanila mjini Manyovu wilayani Buhigwe, leo, Lugola alisema anataarifa za kutosha kuhusu wahamiaji haramu kutoka nchi za jirani wapo mkoani humo, hivyo lazima waondolewe kwa mujibu wa sheria.
Lugola ambaye alikua akishangiliwa na wananchi baada ya kutoa agizo hilo, pia alikemea tabia ya baadhi ya watu wanaohifadhi raia hao wa kigeni ambao wameingia nchini kinyume cha sheria.
 
“Sasa natoa agizo hili na litekelezwe, Uhamiaji mkoa washirikiane na polisi kuwaondoa raia hawa wa kigeni ambao wameingia nchini kwa njia zisizo halali, nataka operesheni hii ianze mara moja,” alisema Lugola.
 
Lugola pia aliirudia kauli hiyo ya kuondolewa kwa wahamiaji hao haramu alipokua anazungumza na wananchi wa Kijiji cha Kalinzi, Wilaya ya Kigoma Vijijini, na kuongeza kuwa anashangaa wahamiaji hao wanaendelea kuwepo mitaani huku maafisa uhamiaji wakiwepo mkoani humo.
 
“Hivi inakuaje, wananchi wanalalamika hapa kuhusu uwepo wa wahamiaji haramu, lakini Uhamiaji mpo, mnakaa kimya tu, mnataka mpaka mimi nije ndio nitoe maelekezo haya? Hii sitaki kusikia tena, nataka operesheni hii ianza mara moja na iwe endelevu,” alisema Lugola.
 
Hata hivyo, Lugola alisema katika operesheni...

HOTUBA YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MHE. DKT. MWIGULU LAMECK NCHEMBA (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2018/19

Thursday, May 3, 2018

 
HOTUBA YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI
MHE. DKT. MWIGULU LAMECK NCHEMBA (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI
KWA MWAKA 2018/19
 

  1. UTANGULIZI

 

  1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu, baada ya kuzingatia taarifa iliyowasilishwa hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, likubali kupokea, kujadili na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka 2018/19.

 

  1. Mheshimiwa Spika, naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia uzima na kuniwezesha kuwasilisha Hotuba ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambayo itajadiliwa na Bunge hili.

 

  1. Mheshimiwa Spika, pia natumia fursa hii kumshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Kwa kuongoza vema Taifa letu Na kuendelea kusimamia amani, utulivu na usalama nchini. Ni dhahiri...

Opening Statement by Hon. Mwigulu Lameck Nchemba (MP), Minister for Home Affairs of the United Republic of Tanzania on the 19th Meeting of the Tripartite Commission for the Voluntary Repatriation of Burundian Refugees in Tanzania held on 31st August 2107,

Thursday, August 31, 2017

 
Hon. Pascal Barandagiye, Minister for Interior and Patriotic Education of the Republic of Burundi and Head of Burundi Delegation,
Madam Chansa Ruth Kapaya, UNHCR Country Representative in Tanzania and Head of UNHCR Delegation,
 
Hon. Brig. General (Rtd) Emmanuel Maganga, Kigoma Regional Commissioner,
Hon. Major General (Rtd) Salum M. Kijuu, Kagera Regional Commissioner, 
Mr. Abel Mbilinyi, UNHCR Representative for Burundi,
 
H.E. Rajabu Hassan Gamaha, the Ambassador of the United Republic of Tanzania in Burundi,
 
H.E. Gervais Abayeho, the Ambassador of the Republic of Burundi in Tanzania,
 
Distinguished Heads of Technical Working Group Delegations,
Distinguished Delegates and Guests,
Ladies and Gentlemen,
It’s my great pleasure to welcome you to Dar es Salaam and to this important meeting of the Tripartite commission for the Voluntary Repatriation of Burundian Refugees in Tanzania. I hope that so far you have enjoyed your stay in this wonderful and great city.
Excellences, Distinguished Ladies and Gentlemen,
As we start the meeting of the Tripartite Commission for the Voluntary Repatriation of Burundian Refugees in Tanzania, I would like at the outset to affirm the commitment...

OPENING SPEECH BY HON. MWIGULU LAMECK NCHEMBA (MP), MINISTER FOR HOME AFFAIRS, AT THE HIGH-LEVEL DIALOGUE BETWEEN THE GOVERNMENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA AND THE UNITED NATIONS HIGH COMMISSIONER FOR REFUGEES (UNHCR)

Wednesday, August 9, 2017

 
 
Hon Rtrd Major General Raphael Mugoya – Regional Commissioner Katavi
Hon Rtrd Brigadier General Emanuel Maganga Regional Commissioner of Kigoma
Ambassador Simba Yahya, Deputy Permanent Secretary, Ministry of Home Affairs
Distinguished Regional Administrative Secretaries
Hon District Commissioners for Ngara
 
Distinguished Senior Government Officials
 
Mr. Volker Turk, UNHCR, Assistant High Commissioner – Protection, Geneva
 
Ms. Catherine Wiesner, Regional Refugee Coordinator (Burundi), Nairobi
 
Valentin Tapsoba, Director, UNHCR Regional Bureau for Africa, Geneva
 
Mr.  Mamadou Dian Balde, Deputy Director, Comprehensive Response CRRF, Geneva
 
Ms. Chansa Ruth Kapaya, UNHCR Country Representative
 
Ladies and Gentlemen,
 
Good morning
 
Allow me at the outset, on behalf of the United Republic of Tanzania and on my own behalf to give a warm welcome to our co-operating partners from the office of the High Commissioner in Geneva to Tanzania and in particular to this high-level dialogue between the government of the United of Tanzania and the United Nations High Commissioner for Refugees (UNHCR).
We are indeed grateful...

STATEMENT BY AMB. HASSAN YAHYA SIMBA, DEPUTY PERMANENT SECRETARY, MINISTRY OF HOME AFFAIRS ON GOVERNMENT OF TANZANIA PERSPECTIVES ON THE PROTECTION AND SOLUTIONS FOR REFUGEES IN TANZANIA DELIVERED AT THE HIGH-LEVEL DIALOGUE WITH THE UNITED NATIONS HIGH

Wednesday, August 9, 2017

 
 
Hon, Mwigulu Lameck Nchemba - Minister for Home Affairs
Hon Rtd Major General Raphael Mugoya – Regional Commissioner Katavi
Hon Rtd Brigadier General Emanuel Maganga Regional Commissioner of Kigoma
Distinguished Regional Administrative Secretaries
Hon District Commissioners for Ngara
Distinguished Senior Government Officials
Mr. Volker Turk, UNHCR, Assistant High Commissioner – Protection, Geneva
Ms. Catherine Wiesner, Regional Refugee Coordinator (Burundi), Nairobi
Valentin Tapsoba, Director, UNHCR Regional Bureau for Africa, Geneva
Mr.  Mamadou Dian Balde, Deputy Director, Comprehensive Response CRRF, Geneva
Ms. Chansa Ruth Kapaya, UNHCR Country Representative
Senior UNHCR Officials
 
Distinguished Participants,
 
Ladies and Gentlemen;
 Good morning.
 
 
It gives me great pleasure to participate in this high level diaologue on key issues on asylum and protection for people that are compelled to seek refuge in our country. On behalf of the Government of the United Republic of Tanzania, I wish to extend my appreciation to the United Nations High Commissioner for Refugees for timely facilitating this...

MAGEREZA KUPANUA KIWANDA CHAKE CHA VIATU CHA KARANGA MJINI MOSHI

Tuesday, July 11, 2017

 
 
Na Christina R. Mwangosi
 
Jeshi la Magereza nchini limeanza kutekeleza mpango wake wa kupanua shughuli za uzalishaji wa kiwanda cha Viatu cha Karanga  kilichopo mjini Moshi  mkoani Kilimanjaro  sambamba na kujenga Kiwanda Kipya cha Viatu  katika eneo hilo hilo ili kupanua huduma zake kwa wananchi na hivyo kukidhi mahitaji ya soko la sasa.
Hatua hii ni moja ya kati ya Mikakati ya Jeshi la Magereza nchini Tanzania linaloongozwa na Kamishna Jenerali Dk. Juma Malewa kuhakikisha fursa  zilizopo na wataalamu waliopo ndani ya Jeshi la Magereza nchini zinatumika na wanatumika  vizuri kwa manufaa ya watanzania wote sambamba na Jeshi hilo kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha Tanzania inafikia uchumi wa viwanda.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dr. Juma Malewa anasema baada ya upanuzi huo ambao umeanza kufanyika mapema mwezi Juni mwaka huu kiwanda hicho kitakuwa na  uwezo wa kuzalisha  jozi 400 kwa siku na hivyo kuongeza kasi ya upatikanaji wa viatu vinavyotengenezwa na Jeshi la Magereza kwa ubora kwa hali ya juu na kwa kutumia mitambo ama mashine  za kisasa.
Dk. Malewa anasema awali  kiwanda  hicho kilichopo Gereza la Karanga mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro kutokana na kutumia teknolojia ya zamani   kilikuwa na  uwezo wa kuzalisha jozi 150 kwa siku kiwango ambacho ni kidogo ukilinganisha na soko la sasa.
Anasema tayari Jeshi la Magereza limeingia Ubia na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PPF   kwa lengo la kupanua ...

MAGEREZA KUFUFUA KIWANDA CHAKE CHA SUKARI NA KILIMO CHA MIWA MOROGORO

Tuesday, July 11, 2017

 
 
 
Na Christina R. Mwangosi
 
Jeshi la Magereza nchini limeanza kutekeleza mpango wake wa kufufua Kiwanda chake cha  Sukari na  Kilimo cha Miwa katika Gereza la Mbigiri mkoani Morogoro kwa lengo la kuongeza kiwango cha upatikanaji wa sukari hapa nchini ikiwemo kutoa fursa za ajira kwa watanzania.
Pamoja na kiwanda hicho kuongeza upatikanaji wa sukari hapa nchini lakini pia kufufuliwa kwa kiwanda hiki kutatoa fursa ya ajira Wananchi ambao watafanya kazi kwenye Kiwanda hicho kwa ujumla.
Katika kutekeleza mpango huo hatua za awali za Upembuzi yakinifu umeshafanyika na shughuli za kilimo tayari zimeanza katika eneo hilo kwa kutumia maktrekta matatu mapya ya kisasa ambayo hadi sasa yameshalima ekari 1000.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Dk. Juma Malewa anasema kuwa katika kutekeleza Sera ya Uchumi wa Viwanda, Jeshi la Magereza limeainisha baadhi ya Miradi inayoweza kuiweka Tanzania katika Uchumi wa Viwanda ikiwemo ufufuaji wa Kiwanda hicho na Kilimo cha Miwa katika Gereza lake la Mbigiri Mkoani Morogoro.   
Dk. Malewa anasema kuwa  kwa kushirikiana na  Mifuko ya Hifadhi ya Jamii PPF na NSSF,  Jeshi la Magereza  limeanza zoezi  la kufufua  Kiwanda cha Sukari na  Kilimo cha Miwa katika Gereza la Mbigiri mkoa wa Morogoro.
Dk. Malewa anasema Kiwanda hicho kilisitisha shughuli zake za uzalishaji tangu mwaka 1996 kutokana na uchakavu wa miundombinu na teknolojia duni iliyokuwepo kwa wakati huo.
...

JESHI LA MAGEREZA KUTOA ELIMU YA NAMNA YA KUANZISHA KILIMO CHA KISASA KWA KUTUMIA MAENEO YENYE UFINYU WA NAFASI

Tuesday, July 4, 2017

 
Na Christina Mwangosi, MOHA
 
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Dk. Juma Malewa amesema Jeshi la Magereza nchini litatoa elimu ya namna kila Mtanzania hata aishie kwenye nyumba za ghorofa ama maeneo yenye nafasi ndogo ya kuanzisha kilimo cha mbogamboga, anavyoweza kutumia eneo dogo kuendeshea shughuli za kilimo cha mbogamboga wakati huu Maonyesho ya SabaSaba yanayoendelea katika Viwanja vya SabaSaba jijini Dar es salaam.
Kamishna Jenerali Dk. Malewa amesema kuwa pamoja na kuandaa Shamba Darasa kwa ajili ya kutoa elimu ya shughuli mbalimbali za kilimo, Jeshi la Magereza  limeandaa bidhaa mbalimbali ambazo zitaonyeshwa wakati wote wa Maonyesho pamoja na kuuzwa wakati wote wa Maonyesho hayo.
Dk. Malewa amesema miongoni mwa bidhaa hizo ambazo ziko kwenye Banda la Magereza ni samani  mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya ofisi na nyumbani ikiwemo makabati ya vyombo na nguo,  meza na viti,  madawati kwa ajili ya shule za  msingi na sekondari, vitanda, sofa, ‘dressing table’  pamoja na viatu vya ngozi vya kike na kiume.
Amesema Jeshi la Magereza pia litauza pia majiko sanifu  yanayotumia kuni kidogo, mashuka, foronya, vikoi pamoja na sabuni zenye ubora kwa ajili ya kufua nguo ambazo zinatengenezwa katika Kiwanda cha Sabuni kilichopo Mkoa wa Mbeya.
Amesema Jeshi la Magereza katika kipindi hiki cha Maonyesho litatoa elimu ya shughuli za kilimo cha kisasa bure na kwa wale wananchi ambao maeneo yao yanafikika...

MAKALA: LEO NI MAADHIMISHO YA SIKU YA WAKIMBIZI DUNIANI

Tuesday, June 20, 2017

LEO NI MAADHIMISHO YA SIKU YA WAKIMBIZI DUNIANI
 
Na Christina Mwangosi, MOHA
Tarehe 20 mwezi Juni ya kila mwaka hufanyika Maadhimisho ya Siku ya Wakimbizi Duniani ambapo Tanzania imekuwa ikiadhimisha siku hiyo kila mwaka huku Maadhimisho hayo yakilenga kuhamasisha mataifa mbalimbali kuendelea kuwahifadhi na kuwahudumia wakimbizi wanaokimbia nchi zao za asili kutokana na machafuko na majanga mbalimbali kama ambavyo Mikataba ya Kimataifa inavyoendelea kusisitiza juu ya kuendelea kuwahifadhi na kuwahudumia wakimbizi .
Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) ambalo kwa hapa nchini hufanya kazi za Kuwahudumia Wakimbizi kwa karibu sana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Idara ya Huduma za Wakimbizi  kwa mwaka huu Maadhimisho hayo yatafanyika jijini Dar es salaam huku kauli mbiu ya mwaka huu wa 2017 ikiwa ni ‘Tupo Pamoja Na Wakimbizi’  ‘We Stand Together With Refugees’
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kuwahifadhi na kuwahudumia wakimbizi ambao wamelazimika kuyahama makazi yao  kwa sababu ya vita na machafuko na kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) kiasi cha watu 43 milioni duniani kote wamelazimika kuyahama makazi yao kwa sababu ya vita, machafuko au majanga ya asili, na kati yao kiasi cha milioni 10 wanahudumiwa na Shirika hilo.
Katika kipindi cha mwaka 2016/17 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa...

MAADHIMISHO YA SIKU YA WAKIMBIZI DUNIANI TAREHE 20 JUNI,2017

Tuesday, June 20, 2017

 
 
 
 
Kila mwaka, tarehe 20 Juni, Mataifa yote ulimwenguni huadhimisha Siku ya Wakimbizi Duniani (World Refugee Day). Awali siku hiyo ilikuwa inaadhimishwa Barani Afrika peke yake ikiitwa Siku ya Wakimbizi Barani Afrika na kuanzia mwaka 2001 Maadhimisho hayo yalianza kufanyika Duniani kote baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuelekeza hivyo katika kuadhimisha miaka 50 ya Sheria ya Kimataifa ya Wakimbizi.
 
Lengo la maadhimisho haya ya kila mwaka ni kuhamasisha Ulimwengu kutambua uwepo wa mamilioni ya wakimbizi na watu wengine wanaohama kutoka kwenye maeneo yao kwenda maeneo mengine ndani ya nchi zao (internally displaced persons) kuogopa vita, migogoro na mateso.
 
Maadhimisho haya huwahusisha viongozi wa serikali, watumishi wa mashirika ya misaada, watu mashuhuri na wakimbizi wenyewe. Maadhimisho haya huambatana na kauli mbiu ambayo kutoa msisitizo wa jambo ambalo hupewa msukumo katika matamko ya mwaka husika ambapo Kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Tuko Pamoja na Wakimbizi’  ikiwa na lengo la kukumbusha jukumu la kila mmoja la kuwasaidia wakimbizi na kutafuta ufumbuzi wa matatizo ambayo yamesababisha wao kujikuta katika hali hiyo.
 
Kama inavyofahamika Tanzania imekuwa na historia ndefu ya kuhifadhi wakimbizi toka nchi mbalimbali za Afrika na kwingineko.  Kwa vipindi mbalimbali wamekuwepo wakimbizi tofauti tofauti kama vile  wakati wa harakati za kupigania uhuru wa nchi za Kusini ya...

Pages

Subscribe to
Back to Top