Tanzania logo

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

KATIBU MKUU MMUYA AWAKUMBUSHA WANAHABARI KURIPOTI HABARI ZENYE KULINDA TASWIRA YA NCHI



Akifugua Semina na Mafunzo kwa Wanahabari za Mitandao na Maafisa wa Kipolisi,Magereza,Uhamiaji ,Zimamoto na Uokoaji,Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA) Leo Disemba 20,2023 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi Kaspar Mmuya amesema Wanahabari pamoja na vyombo vya dola ni muhimu kuwepo kwa Mashirikiano katika Kuhabarisha Umma hasa yanapotokea maafa na majanga katika jamii.

"Mwanahabari anafika katika tukio anapiga picha za kuleta taharuki anasambaza katika mitandao ya kijamii wakati kwa muda huo angeweza kunusuru maisha ya watu pale tukio linapotokea hivyo semina hii itakwenda kubadilisha taswira kwenye jamii kuwa kazi ya kuokoa watu hata Wanahabari wanaweza kusaidia kuliko kukimbilia kupiga picha za taharukina zisizo na utu na staha .

Hata hivyo Mmuya ameongeza kuwa Kama inavyofahamika Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi kupitia vyombo vyake vya Usalama na Idara zake zote ina Jukumu kubwa la Kusimamia usalama na raia na mali zao kuhakikisha nchi yetu inakuwa na amani na utulivu.

"Hivyo hata Uandishi wa habari za matukio yanayohusu Wizara na vyombo vyake vya Usalama hauna budi kuzingatia weledi hivyo kuepuka kuandika habari zenye kuzua hofu ,taharuki ,kuleta vurugu ,uchochezi ama kuondoa amani tuliyo nayo nchini ambazo kwetu ni tunu."

Aidha amebainisha kuwa Wizara hiyo imeona changamoto ya baadhi ya waandishi wa habari ama kwa kujua au kutokujua wanajikuta wanaandika habari za matukio yanayohusu Wizara,Jeshi la Polisi, Magereama Uhamiaji bila kuzingatia maadili ya Uandishi wa habari.

Mmuya ameongeza kuwa Mafunzo hayo ambayo yamefunguliwa rasmi Leo ameyagawa kwa awamu mbili kwa makundi ambapo kundi la kwanza waandishi wa habari za mitandaoni na Kundi la pili litahusisha waandishi wa habari za Magazeti,radio na televisheni ili waweze kufahamu namna ya kuripoti habari inayolihusisha Jeshi la polisi ,Uhamiaji ama Magereza.

Pia amewapongeza Wanahabari kwa kazi zao kwa kuhabarisha umma kwa wakati na kutafuta vyanzo vya habari hizo na kuhusisha Jeshi la polisi kutoa maelezo yaliyo kamili zaidi na kuwaomba kutumia nafasi hiyo ya mafunzo hayo ili waweze kuwajibika kwa pamoja katika jukumu zima la Usalama wa raia na mali zao,Ulinzi na utulivu wa nchi.

Ametoa rai kwa rai kuwasaidia wahanga katika maafa mbalimbali yanapotokea kuliko kupoteza muda kurekodi video au kupiga picha kwa ajili ya kuwahi kuuhabarisha umma kupitia mitandao ya kijamii.

Kwa upande wake Mwenyekiti Jukwaa la Wanahabari za mitandao (JUMUKITA) Shaban Omary amesema Semina hiyo ina lenga kufikisha uelewa na mashirikiano kwa vyombo vya Jeshi la polisi pamoja na Wanahabari katika kuripoti habari mbalimbali.

"Semina hii kikubwa ni kukumbushana na kuelekezwa miiko katika kuripoti habari katika jamii na kuilinda nchi yetu.''

Hata hivyo Amefafanua zaidi kuwa kuundwa kwa umoja wa Wanahabari (JUMUKITA) ilikuwa na lengo kushirikiana katika namna ya kutoa taarifa kwa haraka zaidi na kurinda taswira na maadili ya nchi.

Pia ameomba Semina hiyo iwe endelevu ili kuendelea kutoa taarifa mbalimbali kwa Wanahabari kuripoti kwa usawa na maadili mazuri kw maslahi mapana na nchi.