Get Adobe Flash player
 • Rais Kikwete Awapa Uraia Wakimbizi wa Burundi 162,156 Mjini Tabora

  Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (kushoto) akimuonesha Rais Jakaya Kikwete (kulia) mchoro unaoonesha jinsi wakimbizi wa Burundi walivyoingia nchini wakati walipokuwa wanatoka nchini kwao mwaka 1972

 • Rais Kikwete Awapa Uraia Wakimbizi wa Burundi 162,156 Mjini Tabora

  Rais Jakaya Kikwete akimpa cheti cha uraia wa Tanzania, Loveness Ruhaga (kulia) aliyekuwa Mkimbizi kutoka nchini Burundi katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Tabora

 • Rais Kikwete Awapa Uraia Wakimbizi wa Burundi 162,156 Mjini Tabora

  Rais Jakaya Kikwete akizungumza baada ya kuwapa vyeti vya uraia wa Tanzania, waliokuwa wakimbizi 162,156 kutoka nchini Burundi walioingia nchini tangu mwaka 1972

 • Rais Kikwete Awapa Uraia Wakimbizi wa Burundi 162,156 Mjini Tabora

  Sehemu ya wakimbizi wa Burundi 162,156 ambao sasa ni raia wa Tanzania baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwapa uraia katika halfa iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora. Rais Kikwete amewataka raia hao wapya wawe waadilifu na kufuata sheria zote za nchi

 • Rais Kikwete Awapa Uraia Wakimbizi wa Burundi 162,156 Mjini Tabora

  Rais Jakaya Kikwete (wasita kushoto waliokaa), mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa nchini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (watano kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke (watatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa (wasita kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya raia wapya 162,156 wa Tanzania (nyuma waliosimama) baada ya kupewa vyeti vya uraia na Rais Kikwete katika hafla iliyofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini humo

 • Image2

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) akimsikiliza kwa makini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (katikati) alipokuwa akifafanua jambo wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu ya Zanzibar

 • Waziri Chikawe Kufuta Usajili wa Makanisa Yenye Migogoro kwa Lengo la Kuepusha Uvunjifu wa Amani Nchini

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na maelfu ya Waumini wa Karismatiki Katoliki, Jimbo la Dar es Salaam katika maombi maalumu kwa ajili ya kuliombea Taifa yaliyofanyika Kituo cha Karismatiki, Ubungo jijini Dar es Salaam. Waziri Chikawe alikuwa mgeni rasmi katika maombi hayo aliyataka Makanisa nchini kudumisha amani na utulivu na kuendelea kuliombea Taifa na kuepuka kuingia katika migogoro mbalimbali ambayo itasababisha taifa kuingia katika uvunjifu amani makanisani.

 • Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (kushoto) akizungumza katika hafla fupi ya kupokea misaada ya Pikipiki, Kompyuta na Samani za ofisini ambazo zimetolewa na Serikali ya China

 • Image7

  Msimamizi wa Kiwanda cha Kuzalisha Nyuzi za Mkonge cha Gereza Kihonda lililopo mkoani Morogoro, Fidelis Muhaya akimuonyesha majani ya mkonge ambayo yamevunwa, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (Kushoto). Katikati ni Mshauri wa Masuala ya Jinsia wa Programu ya Sekta ya Sheria nchini, Wanyenda Kutta.

 • Image3

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akitoa hotuba fupi ya kuishukuru Serikali ya Japan kwa kuisadia wizara yake kupitia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji magari matano kwa ajili ya kazi ya kuzima moto na uokoaji nchini.

 • Image4

  Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe, akiangalia moja ya hati zinazotolewa na Uhamiaji, wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Pereira Ame Silima.